Scroll To Top

Kutekeleza Ushindi Wa Kristo Hadi Duniani 4

Sehemu Ya Nne

Na Jacquelyn Fedor

Ilitafsiriwa Na David Odhiambo
2014-03-31


Tafadhali bofya maandishi ya samawati hafifu kwa maelezo zaidi


Kwa wale ambao mmekuwa mkifuatilia mfululizo huu inatupasa kufikia sasa kuelewa kikamilifu kwamba kuna falme mbili tofauti kabisa, vyanzo viwili tofauti kabisa vya maarifa vinavyopatikana kwa mwanadamu, na aina mbili tofauti au spishi za mwanadamu zilizopo leo. Moja inahusiana kijeni na Walinzi, ambao ni malaika wa Mungu na Adamu, na nyingine inahusiana na Baba na Hekima, ujuzi wa Mungu kupitia kanisa. Hebu nielezee.
Yakobo 1:18 inasema,
18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno la ukweli, ili tuwe namna ya malimbuko ya viumbe vyake. (Tunajua jamii ya Adamu ilikuwepo maelfu ya miaka kabla ya kauli hii kutolewa, lakini hata hivyo Yakobo alikuwa anazungumza juu ya kizazi chake kuwa malimbuko. Anasema Neno, Kweli inatubadilisha kuwa aina tofauti.)
Sisi pia tulitolewa, au tulizaliwa kupitia Neno lililotolewa kwa enzi hii ya kanisa Lake. Mungu amekuwa akifichua kwa uthabiti mpango Wake wa urejesho wa mwanadamu katika kila enzi. Mwanadamu anapoelewa maarifa yaliyoachiliwa, ukweli mpya ungeweza kufichuliwa ambao ungeongoza ubinadamu hatua kwa hatua karibu na ukamilifu wao wa asili. Wale wanaosikia ukweli, kuuamini na kuanza kuutembea wanakuwa aina tofauti ya ubinadamu, mlimbuko wa enzi hiyo. Katika enzi hii wanadamu wanaanza kuelewa kwa kweli kiwango cha kile kilichotokea kwa Adamu na Hawa. Shetani katika jitihada yake ya kuwa kama Mungu, au kuwa kama Mungu kwa viumbe, kwa hila alimvuta Hawa katika uasi dhidi ya mapenzi ya Baba. Mfuniko wake, Adamu, kilifuata katika uasi wake na kwa pamoja wakasalimisha akili zao kwa adui wakikubali elimu yake, na kumpa Mungu kisogo. Hawakuwa wameunganishwa tena na akili ya Mungu walikuwa uchi wa kiroho na kimwili na peke yao, kutoka chini ya ulinzi wa sheria ya Mungu, nje ya utaratibu Wake aliokusudia, na wote waliokuwa wamepewa kuwa watunzaji waliteseka vibaya sana katika kushindwa kwao pia. Kwa hivyo inabakia leo.
Uumbaji unatutegemea sisi na hutungoja kwa hamu tukue katika ujuzi, tukomae hadi mahali tuwe tayari kwa mavuno ya mwisho. Wakati sisi, malimbuko ya wakati huu tunapotengwa na kuwekwa pembeni kabisa na jamii nyingine, yote ambayo ni ya Mungu na yote tuliyopewa yatawekwa huru kutoka kwa ulimwengu wa Shetani na mifumo yake. Ulimwengu huu wa magonjwa, maumivu, ufisadi na kifo utaharibiwa hivi karibuni. Kweli kila kitu na kila mtu ameteseka kwa mkono wa Shetani hapa duniani. Lakini, mavuno ya nakuja! Mbegu njema itatengwa, kutiwa nanga, kukatiliwa mbali na waovu, yote ni ufafanuzi wa neno mavuno, na kuwekwa kando, waovu wataangamizwa.
Mathayo 13:49-50 inathibitisha hili.
49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa nyakati. Malaika watatokea, watawatenga waovu kutoka kwa wenye haki,
50 na kuwatupa katika tanuru ya moto. Kutakuwa na kilio nakusaga meno.”
Waovu watakuwa hawajalindwa kwani sheria ya Mungu ni nuru inayoangaza njia kwa uzao mtiifu wa Mungu tu, ufahamu wa Shetani unafundisha kwamba sheria zinafunga, zinakuweka mfungwa, lakini ujuzi wa Mungu hutusaidia kuelewa kwamba sharia hutupa uhuru kutoka kwa adui, ulinzi kutoka kwa uovu, mwelekeo kwa kutembea kwetu kila siku. Fikiria njia nyembamba ambayo pande zote mbili kuna nyoka wenye sumu. Kuna giza. Sharia ni nuru inayo tuambia ni namna gani ya kuendakukaa kwenye njia iliyo salama. Inategemea, lakini haijafungwa, inalindwa sio kufungiwa, kuelekezwa lakini si wajibu wa kuwa mtiifu. Sio njema ikiwa hatuzijali au tunakataa kutii. Hii ndiyo njia ya sharia ya Mungu. Anatupenda sana aliyaandika sharia zake mioyoni na akilini zetu ilikuyafikia kwa urahisi. Angalia hiyo sio sharia ya Musa. Ni sharia waliyopewa viumbe wake wapya ili kuwaongoza.
Waebrania 10:16 inaeleza sheria hizi.
16 “Hili ndilo agao nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sharia zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.”
Mwanadamu amefungwa kwa adui bila njia ya uhuru bila wao. Ukuu wa Mungu unaunga mkono sharia yake, unasimama imara milele, haubadliki wala hauonyeshi upendeleo. Sharia inamweka mwandamu hurukutokana na roho ya uraibu, uwoga, wasiwasi, udhaifu n.k. Jamii ya Adamu inashikiliwa nao kabisa. Wao kwa namna fulani ni wa roho hao waovu nani watumwa wao, vikaragosi wao, hasa kwa sababu wao ni maskini sana katika ujuzi wa Mung una wamezama sana katika ujuzi wa ulimwengu. Pia wanahusiana kijeni na waovu wanaowadai. Kwa hiyo adui ameshikamana na yote waliyonayo katika miliki yao hadi Mungu atakapoamua kuikomboa dunia yote katika jubilee ya mwisho. Wakati huo maskini wanaompenda na kufanya bidi yao yote kushika amri zake watawekwa huru na pia kuhifadhiwa ili wafundishwe katika kipindi cha milenia.
Tunaweza kuona hii katika Walawi 25:13, 25, 28
13 Katika mwaka huu wa jubilee, kila mmoja atarudishiwa miliki yake (tulikuwa na miliki ya dunia na vyote vilivyomo)
25 ‘Ikiwa mmoja wa ndugu zako amekuwa maskini (katika ujuzi), na ameuza sehemu ya mali yake (Adamu na Hawa waliuzwa kwa Shetani), na jamaa yake mkombozi (Kristo) akija ili kuikomboa, ndipo anaweza kukomboa kile ambacho ndugu yake aliuza.
Hiki ndicho ninachotaka tuone kwani ni sheria.
28 Lakini ikiwa hana uwezo wa kuikomboa (hakuna maarifa ya kutosha juu ya Kristo kubadilika), basi kile kilichouzwa kitabaki mkononi mwa yule aliyekinunua (Shetani) mpaka Mwaka wa Jubile; na katika Jubile itaachiliwa, na yeye (ampendaye Mungu) atarudi kwenye miliki yake (na kufundishwa katika milenia).
Jubile ni kubwa kwa watu wa Mungu, ni nzuri pia kwa wale waliohifadhiwa ili kujifunza, lakini kuwaangamiza wasio na sheria na adui wa Mungu. Acheni tumtazame vizuri Shetani kwa kuwa yeye ndiye mkuu wa ulimwengu huu, kiongozi wa pepo wachafu wanaomsumbua mwanadamu leo na kamanda na mkuu wa kundi lake la waasi-sheria.
Isaya 14:12-15 inafunua tabia ya Lusifa au Shetani.
12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe Lusifa, mwana wa asubuhi! jinsi ulivyokatwa chini, wewe uliyeyadhoofisha mataifa, (uliowavusha pamoja na malaika, ukawagawanya makundi, jinsia, madhehebu, dini za siri, makundi ya siri n.k.)
13 Kwa maana umesema moyoni mwako, 'Nitapanda mbinguni, nitainua kiti changu cha enzi juu ya nyota ya Mungu; nami nitaketi katika mlima wa kusanyiko (anataka kutawala watu wa Mungu kutoka mlima wake mtakatifu) katika pande za mbali zaidi za kaskazini;
14 Mimi nitapanda vilele vya mawingu nitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu,” (Nita mara tano, nikionyesha ubinafsi na kiburi cha kiumbe hiki!)
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu, utashushwa chini kabisa shimoni.
Tunaona utimilifu aya ya 15 Ufunuo 20:1-3
1 Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akalikamata jile joka-nyoka wa kale, yaani ibilisi au shetani-akalifunga kwa mda wa miaka 1000
3 Malaika akilitupa kuzimu, akafunga mlango wa kuingilia huko na kuitia muhuri ili lisiweze tena kupotosha mataifa mpaka hapo miaka 1000 itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu. (sababu ni hii)
Wale wanaotunzwa kwa ajili ya kukamilishwa katika kipindi cha milenia lazima pia wazaliwe mara ya pili na kuchagua mti wa uzima mbele ya yule aliyewadanganya Adamu na Hawa. upendo wao kwa Mungu lazima uthibitishwe katika uso wa yule aliyejiona kuwa mwenye hekima zaidi, mwenye nguvu zaidi kuliko muumba wake. Hivyo shetani atafunguliwa kwa muda kidogo ili kuwajaribu. Mungu anasema “wale wanipendao watashika amri zangu”. Sheria hiyo itawahukumu wakati huo, kama vile tunavyotazamwa kwa karibu sasa, Adui na Mungu wanatuangalia kwa makini, kama vile kuna falme mbili, maarifa mawili ya kuchagua, kuna miili miwili inayoinuliwa, Mwili wa Kristo na mwili wa Shetani.
Yesu anapoingiliana kupitia mwili wake, ndivyo shetani anavyoingiliana kupitia mwili wake. Wale wa mwili wa Kristo ni watiifu kwa sharia ya Mungu, wana huruma kwa watu wa ulimwengu na wanatamani kuwaona, pamoja na viumbe vyote, wakirejeshwa na kurudishwa kwa Muumba. Wale wa mwili wa shetani, kama vile bwana wao, ni wahalifu, wanajishughulisha tu na maisha yao bila kujali sayari yenyewe au kitu chochote kilicho juu yake. Kwa kweli bwana wao anataka kuharibu vitu vyote ambavyo Mungu ameumba. Hivi sasa miili hiyo miwili inafanana sana. Huwezi kutofautisha ngano na magugu, lakini hii inabadilika haraka. Mbingu na kuzimu vinagombana. Miili miwili tofauti kabisa inabadilika katika asili, mtazamo, hata muonekano. Wanazidi kudhihirika wao ni nani. Mungu anaachilia ukweli ili kufungua macho yetu, na kutuwezesha kujitambua sisi ni nani na sisi ni sehemu ya mwili gani. Wengi wamedanganywa, wakadaiwa na shetani na kukamatwa bila hatia katika mwili usiofaa. Mungu anawaita watengane leo na kuwakaribisha kwa mikono miwili kuwa sehemu ya jamii yake ya viumbe vipya waliozaliwa mara ya pili kupitia Neno.
Hii ndio jambo kuu linalowatenganisha, upendo wao kwa ukweli na utii wao kwa upendo wa dhati kwa Mungu na uumbaji wake. Upendo ndio jambo kuu, huruma huichochea. Upendo ni mshipa unaoshikilia mwili pamoja. Maarifa ni mwili wa Neno au Kristo, na kuwa tofauti hutufunga pamoja na Mungu, na kuumba mfupa, kwa hiyo sisi ni kama mwili wake, nyama ya nyama yake na mfupa wa mfupa wake pamoja na nguvu ya upendo kama mwuongozo. Kwa maneno mengine Mungu ameumba mwili mwingine ili Yesu akae, wakati huu kurejesha dunia nzima. Yesu , kama torati iliyo hai anakaa ndani ya mioyo yao na kuunganishwa na akili zao. Hawa ni watiifu kwa torati, sharia na kuzishika amri zake. Huu ndio mwili halisi wa Kristo uliyozaliwa kwa njia ya Hekima na Bwana. Angalia nilisema “mwili wa Kristo”, hali ya umoja, ingawa washiriki ni wengi. Sasa ngoja nikutambulishe kwa yule muasi, anaichukia Torati, anaichukia Sheria, anamchukia Kristo! Yeye ni mwili wa shetani, kupitia viungo vingi, vinavyosemwa kwa kimoja. Mpinga Kristo!
Tunasoma kuhusu hii mwili katika 2 Wathesalonike 2:3-4
3 Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yeyote ile. Maana siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule uasi utokee (wale wanao kata Neno, wanao kata kubadilika) na yule mwovu aonekane, ambaye mwisho wake ni kuagamizwa kabisa. (Mpinga-Kristo),
4 anayepinga na kujiinua juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, hata anaketi kama Mungu katika hekalu la Mungu, akijionyesha kwamba yeye ni Mungu (Ni wapi tumesikia maneno hayo hapo awali? Je! inaweza kuwa katika Isaya 14?)
Mwili huu unazaliwa kupitia uongo na mafundisho ya uongo ya Babeli. Babeli ni mama ya kila kitu kinachopinga Ukweli, Neno, na Kristo. Anaonekana kuwa mtu wa kidini kwa njia nyingi tofauti, akiwapumbaza wengi. Mume wqke ni shetani. Kwa pamoja wamezaa yule muasi, mwili wa shetani. Kupitia mwili huu anatarajia kufikia malengo yake maovu na kutawala kama Mungu.
Tuendele katiak 2 Wathesalonike 2:8-12 tuone mwili huu vizuri.
8 Ndipo atafunuliwa yule mwasi (tunamfunua) ambaye Bwana atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake (kwa sifa na maombi ya mwili wake) na kumangamiza kwa mng’ao kurudi kwake (anapokuja, akiangaza sheria kama nuru, na kuiangazia dunia kwa maarifa).
9 Kuja kwake yule muasi ni sawasawa na utendaji wa Shetani, kwa uwezo wote, na ishara, na maajabu ya uongo (hila, Shetani ndiye mtabiri mkuu),
10 Na kwa udanganyifu wote wa udhalimu (pazia ya udanagnyifu iko juu ya asilimia kubwa ya watu wa Mungu) kati ya wale wanaoangamia (wale wanaokataa mti wa uzima, Yesu) kwa sababu hawakupokea upendo wa ukweli (katika Isaya Mungu anatuambia watu wake wanakufa kwa kukosa maarifa na anawakataa kwa sababu walimkataa), ili wapate kuokolewa (tusipoipenda kweli, na hatutakubali itubadilishe tutapotea na kuasi sheria).
11 Na kwa ajili ya hiyo Mungu atawaletea upotovu mwingi, ili wauamini uongo (tazama Mungu anawaruhusu wale wanaokataa hekima yake, Hawa aliaminiuongu huo pia),
12 ili wote wahukumiwe (au kulaaniwa) ambao hawakuamini ukweli lakini walikuwa na furaha katika udhalimu (hawakutaka kubadilika).
Falme mbili tofauti, maarifa mawili tofauti kabisa, spishi mbili za wanadamu, miili miwili tofauti ya watu inayounda majeshi tofauti, na makamanda wawili tofauti sana! Nabii anayejulikana sana alitunga kifungo hiki, “mbingu na kuzimu zitakutana uso kwa uso kupia jamii ya wanadamu”. Unabii huu unatimizwa!
Unabii mwingine utakuja kutimia pia, Ufunuo 17:14.
14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana-Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme; na walio naye wanaitwa wateuliwa na waaminifu(Wale wanaounda mwili wa Kristo.)
Tunaweza kujumuisha Ufunuo wote kwa kuwa wote ni ujumbe kwa sasa, lakini nadhani tunapata ujumbe. Itakuwa ni Bwana kupitia mwili wake, Mwili wa Kristo, umoja, akimaliza vita mara ya mwisho dhidi ya Shetani na mwili wake, umoja. Mwili wa Kristo dhidi ya Mpinga Kristo.
Kwa kumalizia, kuwa sehemu ya Mwili wa Kristo lazima tuwe utimilifu wa Waefeso 4:13-16.
13 mpaka sisi sote tufikie umoja wa imani (maono moja yanayotegemea ukweli kufanyiza mwili) na wa hekima wa Mwana wa Mungu (tumechagua ujuzi wake juu ya ulimwengu), kwa mtu mkamilifu (aliyerudi kwa sura yake), kwenye kipimo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja wa njama za udanganyifu, (na Babeli au Leviathan, bibi-arusi wa Shetani),
15 bali tuishike ukweli katika upendo, (ukweli huwaweka huru wale wanaoipokea kutoka kwa ulimwengu huu na adui), na kukua katika mambo yote, katika kwa yeye ambaye ndiye kichwa-Kristo
16 Ambaye kutoka kwake mwili wote ukiunganishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri itendayo kazi ifaavyo (tunatimiza sehemu yetu tuliyopewa katika mwili na kufikia lengo lake). Ambayo kwa hiyo kila kiungo hushiriki sehemu yake (huenenda kwa uaminifu katika yale tuliyoitiwa), hukuza mwili (kukomaa na kufanya kazi kubwa kuliko alipotembea duniani hapo awali) kwa ajili ya kujijenga yenyewe (kusaidiana kufikia hatima yao) kwa upendo (si kwa roho ya mashtaka ya ndugu).
Wakati huu mwili unapofanya kazi pamoja kwa mafanikio, Kristo kupitiia sisi atakuwa tayari kushinda mwili wa shetani na kutekeleza ushindi wa Kristo duniani.
Bofya vichwa ili kucheza nyimbo zinazohusiana na mada hii
Move Over Antichrist
Children Of Light
Final Fight